
Afrobarometer ni shirika lisilo la kiserikali, lisilo la kisiasa ambalo linafanya tafiti za maoni ya umma katika zaidi ya nchi 40 barani Afrika kuhusu masuala ya demokrasia, uchumi, huduma za jamii, utawala, na masuala ya kijamii . Shirika hili limefamnya utafiti dhidi ya Utawala wa Raisi wa Muungano wa Tanzania Mh. Samia
Kutoa sauti halisi za wananchi katika uchukuaji wa sera na kuboresha uamuzi wa serikali ndio lengo moja wapo la shirika la Afrobarometer ambalo makao makuu yake yapo Accra nchini Ghana ,Utafiti uliofanywa na taasisi ya kitafiti ya Afrobarometer mwaka 2024 inaonesha kuwa Rais Samia anakubalika kwa asilimia 83 miongoni mwa wa Tanzania.
Kwa mujibu kwa utafiti huo wananchi wengi waliohojiwa walisema wana imani na Rais Samia kutokana na jitihada zake mbalimbali za kiuongozi alionesha katika kuwaletea maendeleo kwenye nyanja tofauti tofauti ikiwemo maji, elimu, sheria na miundombinu.