
Takribani wananchi milioni 6 wanajishughulisha na uvuvi na wanahitaji nyenzo hizi muhimu kwa usalama wao. Mpango wa serikali ni kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya uokozi na huduma za dharura majini, ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa salama anapokuwa kazini au safarini.
Ni faraja kubwa kuona Boti ya Utafutaji na Uokoaji imeshushwa rasmi kwenye maji ya Ziwa Victoria mkoani Mwanza, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2020–2025. Hatua hii inalenga kuhakikisha usalama wa maisha ya wananchi, hususan Kwa wavuvi,Abiria wa vivuko na mitumbwi,Wafanya biashara ndogondogo,Na shughuli za usafirishaji wa mizigo zinazotegemea ziwa hilo.
Jambo hili lina Maana Kubwa kwa Wananchi, Ziwa Victoria ni chanzo muhimu cha ajira, chakula na usafiri kwa mamilioni ya Watanzania na jirani zao kutoka Kenya na Uganda. Uwepo wa boti ya kisasa ya uokoaji:
Unapunguza athari za ajali za majini,Unaongeza imani kwa wananchi kutumia maji kama njia ya uchumi,Unaunga mkono juhudi za serikali za kuimarisha miundombinu ya uchukuzi majini.
Swala hili ni moja ya shuguli za utekelezaji wa Ilani ya CCM, chama tawala nchini Tanzania ,Katika Ilani ya CCM ya 2020–2025, serikali imejikita kwenye, Kuboresha usafiri wa majini,Kuwa na vifaa vya kisasa vya uokoaji,Kuhakikisha maisha ya wananchi hayapotei kwa uzembe au ukosefu wa maandalizi.Uzinduzi wa boti hii ni ishara ya utekelezaji wa ahadi hiyo, na kielelezo cha uwajibikaji wa serikali kwa wananchi wake.
Hili ni hatua chanya inayopaswa kupongezwa – kwani inawagusa moja kwa moja wananchi wa kipato cha chini na wa kati, wanaotegemea Ziwa Victoria kama sehemu ya maisha yao ya kila siku. Serikali inapaswa kuendeleza jitihada hizi kwa kuhakikisha kuwa,Mafunzo kwa waokoaji yanaendelea,Mitambo na zana zinatunzwa ipasavyo,Na ushirikiano na jamii unaimarishwa kwa utoaji wa taarifa mapema wakati wa dharura.