
Kama tungekuwa na uwezo wa kurudisha siku nyumba safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ilichukua saa tisa hadi kumi za taabu na kuvimba miguu ukiwa kwenye usafiri wa basi...
Tulisafiri kwa taabu na dhiki kubwa huku tukipoteza muda mrefu kwa kuhesabu miti ikirudi nyuma. Tulilala na kuamka zaidi ya mara saba, ndio kwanza tulikuwa tunavuka Daraja la Kiyegeya kuitafuta Gairo, Dodoma.
Rais Samia Suluhu Hassan amedhihirisha dhamira ya kweli ya kuleta mapinduzi ya miundombinu nchini, husu sani katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi. Mojawapo ya mafanikio hayo ni utekelezaji na uendelezaji wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya Umeme (SGR).
Kabla ya mradi huu, wananchi walitegemea reli ya metriki. Ni iliyokuwa imechakaa, ambapo safari kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ilichukua hata zaidi ya saa kumi.
Agosti mwaka 2024 ilizinduliwa rasmi huduma ya treni ya kisasa ya umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, hatua iliyotoa unafuu mkubwa kwa watumiaji wa usafiri huo.
-
Dhamira ya kweli, utekelezaji na uendelezaji wa SGR ndio unawafanya hata baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa na wale wasioitakia Tanzania maendeleo waliokuwa wakise ma ‘SGR haitakamilka’ nao sasa ‘wanakwenda stesheni kupiga picha’.