
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua kikao cha viongozi wa TRA katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (IACC),Kikao hichi chenye malengo makubwa yenye maslahi mapana ya nchi na pia ...
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 08, 2025 anafungua kikao kazi cha Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (IACC).
Kikao hicho kinatoa nafasi kwa viongozi na watumishi wa TRA kufanya tathmini ya kazi, kuona wapi imefanya vizuri, wapi kuna mapungufu na kujiwekea mikakati ya kuimarisha utendaji katika mwaka mpya wa fedha. Kikao kina lengo malengo makuu husika Kupitia utendaji bora wa ukusanyaji,Kujadili mikakati ya kuongeza mapato ya serikali,Kuongeza ushirikiano kati ya TRA, wizara za serikali na wadau mbalimbali.