MAKALA :  MKOPO WA TZS 23.3 TRILIONI HAUJAWAHI KUOMBWA NA RAISI SAMIA

Pamoja na kwamba TZS2.67Trilioni , TZS11.3Trilioni na TZS9.3Trilioni zinazofanya jumla ya TZS 20.6Trilioni zinazoonekana kwenye deni la Taifa la wakati huu wa Serikali ya awamu ya Sita lakini si fedha zilizoombwa na Serikali ya awamu ya 6 kwa maelezo yafuatayo;

Kwanza, Mtakumbuka hadi kufikia Mei 2025, deni la Serikali lilifikia TZS107.70Trilion, Kati ya deni hilo, deni la nje TZS72.94Trilioni na deni la ndani ni TZS34.76 trilioni kati ya hizo jumla ya TZS11.3trilioni ikiwa ni mikopo iliyosainiwa na awamu zilizopita.

Pili, Sababu nyingine ya ongezeko la deni la nje ni kuimarika kwa dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya Tanzania, Kwa mfano mwezi Machi 2021 kiwango cha kubadilisha shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani kilikuwa TZS2,298.5 wakati Machi, 2025 kilikuwa TZS2,650.

Hivyo, endapo deni la serikali litatajwa kwa shilingi ya Tanzania ni lazima lionekane limeongezeka mathalani kwa sasa deni limeongezeka kwa zaidi ya TZS9.3Trilioni. Hatua hii ya kushuka kwa thamani kwa shilingi dhidi ya dola ya Marekani isichukuliwe kama ni hatua hasi bali ilikuwa ni hatua muhimu ya kukabiliana na mtikisiko wa uchumi wa Dunia.

Tatu, Sababu nyingine ya ongezeko la Deni la Serikali la Ndani limechangiwa na mikopo ya kugharamia miradi ya maendeleo na kulipa madeni ya ndani yaliyoiva kwa wawekezaji wa Dhamana za Serikali kwa utaratibu wa kulipia mtaji wa dhamana za Serikali zilizoiva.

Aidha, tulifanya maamuzi ya kutambua madeni mengine ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa Serikali kupitia hatifungani maalumu isiyo taslimu yenye thamani ya TZS2.67 Trilioni kati ya kiasi hicho TZS2.18Trilioni madeni ya PSSSF ya waliokuwa wafanyakazi wa Serikali kabla ya 1999 (maarufu kama pre- 99). TZS433.7bn ni madeni ya NSSF ya muda mrefu na TZS63.52bn ni madeni ya kampuni ya Ubia ya mifuko ya Pension yaani PPP (Pension Property Limited)

Kampuni hii ilifadhili miradi ya Serikali kwa kutoa mikopo kwa vipindi tofauti kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya Serikali ambayo ni ujenzi wa ukumbi wa Bunge-Dodoma na ujenzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Arusha. Madeni haya hayakuwahi kuwa sehemu ya deni la Serikali.

SHUKURANI KWA MCHAMBUZI WETU ; Ibrahim Mkinga  kutoka ST BONGO DIGITAL. 

Kwa habari mbali mbali na udadavuzi wa maswala ya kisiasa na jamii kwa ujumla ,Usikose Kutazama The Bantu Kila siku Jumatatu mpaka Ijumaa Kuanzia saa 10 Kamili mpaka 12 Jioni ndani ya @stbongotv kupitia kisimbuzi cha @startimestz CH 161(antena) CH 401 (Dish) na YouTube Channel yetu ya #STBongoTV


Share: