UWAGIZAJI WA MAGARI UMEKITHIRI KUFIKA KUFIKIA SHILINGI TRILIONI 5 KWA MWAKA

Mabadiliko haya yanaweza kutafsiriwa kwa njia kadhaa, ikiwemo ,

Katika kipindi cha takribani miaka mitatu, thamani ya magari na vifaa vingine vya usafiri vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi imeongezeka kwa kasi kubwa, kutoka shilingi Trilioni 1.9) hadi kufikia shilingi Trilioni 5 kwa mwaka. Ongezeko hili ni sawa na asilimia 20.4, au shilingi Trilioni 3.1 zaidi ya kiwango cha mwanzo.Kuongezeka kwa uhitaji wa vyombo binafsi vya usafiri, kwa ajili ya biashara, huduma za usafirishaji, au matumizi ya familia.

Utamaduni mpya wa Watanzania kuzingatia namba au mwaka wa gari, ambapo baadhi ya watu hubadilisha magari mara kwa mara ili kwenda na wakati au kuongeza hadhi ya kijamii.Urahisi wa upatikanaji wa magari kutoka nje, hasa kupitia njia za kidigitali na mikopo nafuu kutoka taasisi binafsi.


Hata hivyo, mwelekeo huu unafungua mjadala kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika kusimamia ongezeko la magari nchini, hasa kwa kuzingatia athari kwa miundombinu, mazingira, na matumizi ya fedha za kigeni. 


Share: