BILIONI 24 KUJENGA BARABARA YA WASO - LOLIONDO.

Aliwahikuwa Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es salaam na sasa anatumikia vyema nafasi ya mkuu wa mkoa wa Jiji la Arusha na hii ni moja ya tarifa inayo sibitisha uchapa kazi na utekelezaji wa Mheshimiwa Makonda chini ya Uwongozi wa Rais Samia ...

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda,  Juni 9, 2025 ameshuhudia hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Waso hadi Loliondo yenye urefu wa km 10, wilayani Ngorongoro.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Makonda amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua madhubuti katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, hususan sekta ya miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Arusha.


Amemtaka mkandarasi wa China WU Yi Ltd anayetekeleza mradi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi ndani ya kipindi cha miezi 12 kama ilivyopangwa.


Aidha, usanifu wa barabara hiyo ulianza mwaka 2012, na sasa utekelezaji wake unaanza rasmi chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, jambo linalodhihirisha dhamira ya Rais Dkt. Samia ya kufungua fursa mpya za maendeleo kwa wananchi wote.

Share: