Milioni 960 za maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru zilivyoboresha elimu.

Mil 960 za maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru zilivyoboresha miundombinu ya shule za watoto wenye mahitaji maalum.

Katika maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania mwaka 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliekeza fedha zilizotengwa kwa ajili ya Sherehe za Uhuru kwa mwaka 2022 zipelekwe Tamisemi kwa ajili ya kujenga mabweni kwenye shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Fedha hizo zilikua Shilingi Milioni 960 na zilielekezwa kwenye shule 9 zenye uhitaji mkubwa wa mabweni ambazo ni Buhangija iko Shinyanga Manispaa, Idofi ipo Makambako, Longido iko Halmashauri ya Longido, Mtanga iko Kilwa, Goweko ipo Uyui, Darajani ipo Mkalama, Songambele iko Simanjiro pamoja na Msanzi ipo Kalambo mkoani Rukwa.

Napenda kumjulisha Mhe. Rais na umma wa watanzania kuwa ujenzi wa mabweni kwenye shule tajwa umekamilika na nitumie fursa hii kumshukuru Mhe.Dkt.  Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na mapenzi makubwa kwa watanzania wote hususani ni kwa Watoto hawa wenye mahitaji maalum."Mohamed Mchengerwa waziri Tamisemi aelezea.

Share: