Bilioni 190.57 kufanya ununuzi wa magari 113 ya viongozi na kukarabati na kukamilisha miundombinu ya mikoa 26

Serikali imepanga kutumia Tsh. Bilioni 190.57 katika ununuzi wa Magari 113 ya Viongozi wa Mikoa na Wilaya, Kuendelea na Ujenzi, Kukarabati na Kukamilisha Miundombinu ya Mikoa 26 ikiwemo majengo ya Utawala, Ikulu Ndogo, Makazi ya Viongozi na Watumshi wa Mikoa, Wilaya na Tarafa

Waziri Mohamed Mchengerwa wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amesema "Shughuli zitakazotekelezwa katika Utawala Bora ni ununuzi wa Magari 9 ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, Magari 56 ya Wakuu wa Wilaya na 47 ya Wakurugenzi wa Halmashauri”

Share: