WEMA SEPETU KUVAA UCHI ,AITWA NA BODI YA FILAMU TANZANIA

Wema ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne wa mwanadiplomasia Abraham Sepetu. Alianza elimu ya msingi na hadi sekondari amesomea katika shule moja tu iitwayo "Academic International" iliyopo maeneo ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Pamoja na yote hayo, binti huyu amelelewa na kuishi kama mtu wa Magharibi. Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Ubunifu wa Teknolojia cha Limkokwing nchini Malaysia kusoma kozi ya biashara za kimataifa ambayo alisoma kwa mwaka mmoja, kisha akakatisha masomo ili kuendelea na uigizaji. Kipaji zaidi cha Wema kiligundulika katika sanaa ya filamu, ambapo alifanikiwa kucheza vema kabisa katika filamu A Point of No Return akishirikiana na mchezaji filamu maarufu wa Kitanzania Steven Kanumba. Wema alivishwa pete ya uchumba na msanii maarufu wa Bongo Flava Diamond Platnumz, lakini kwa sasa wameshaachana. Pia Wema amekuwa akijulikana kwa kuwa na sauti ndogondogo.

Mrembo ambae pia ni muigizaji kutoka kiwanda cha filamu tanzania @wemasepetu ametakiwa kufika Ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania inayo simamia maadili na nidhamu kwa wasanii wa tasnia hiyo, kufuatia video clip iliyosambaa mitandaoni kumuonesha katika mavazi yanayotajwa kutokua na stara.



Barua ya wito huo imemtaka kuitikia wito mnamo tarehe 22 Mei ili kulinda maadili ya kazi za sanaa na mienendo ya wasanii wake kijamii.

Share: