Issa Tambuu amlipua Chief Godlove gari analomiliki ni million 100
Miongoni mwa mijadala inayoendelea kushika kasi katika mitandao ya kijamii ni kuhusu gari la Chief Godlove ambalo kasema kalinunua kwa shillingi Billion 1.5 baada ya gari hilo kutumika katia Tamthiliya ya "Fast and Furious" ya HollyWood ndipo akaja kulinunua yeye kwa Billion1.5 za kitanzania.
Mfanyabiashara mkubwa wa magari nchini Tanzania Issa Tambu aingilia kati swala hilo na kuliweka wazi ili watu wasiendelee kupotoshwa zaidi.
Akizungumza na StBongo TV Issa amesema kuwa gari aina kama lile la Chief Godlove bei yake kwasasa ni Million95 na usafiri kila kitu haiwezi kuzidi Million100, Swala la Billion 1.5 za chief Godlove yeye hajui imetokea wapi.
Share: