
Rapa kutoka Memphis, GloRilla, amejibu tetesi za mashabiki waliodai kuwa amefanyiwa upasuaji wa kubadilisha sura yake.
Kila kitu kilianza pale shabiki mmoja alipoweka maoni kwenye mtandao wa X akidai kuwa GloRilla alipata kile kinachoitwa “facial balancing” na kuongeza kuwa ilikuwa ni pesa iliyotumika vizuri. Shabiki huyo alieleza kuwa macho yake yalionekana yamewekewa usawa na pua yake kufanyiwa marekebisho, kisha akamalizia kwa kumpa sifa, akimwita mrembo.
Baada ya ujumbe huo kusambaa, GloRilla aliutazama na hakusita kujibu kwa kifupi lakini kwa ukali, akimwambia shabiki huyo kuwa ni “delusional,” akikanusha vikali uvumi huo.
Wakati tetesi hizo zikienea, GloRilla ameendelea kuwa gumzo mitandaoni, si kwa muziki tu bali pia kwa maisha yake ya kibinafsi. Hivi karibuni alithibitisha mahusiano yake na nyota wa kikapu, Brandon Ingram, ambaye anachezea Toronto Raptors. Wawili hao waliweka wazi uhusiano wao kupitia Instagram baada ya muda mrefu wa minong’ono kutoka kwa mashabiki.
Ingram alichapisha mfululizo wa picha wakionekana wakiwa pamoja katika usafiri wa kibinafsi, akifuatisha na maneno yenye ishara ya upendo kwenye maelezo ya picha. GloRilla naye hakusita kujibu, akiweka emoji tatu za macho yenye mapenzi, kitu kilichothibitisha rasmi kuwa wawili hao wako kwenye mahusiano.