Burna Boy awakosoa wasanii wa Nigeria wanao bweteka

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Burna Boy ametoa onyo au kuikosoa tasnia ya muziki Afrika baada ya kusema kuwa "kuwa maarufu kwenye Twitter au kusikilizwa mara milioni moja Nigeria hakutoshi" kwani hakulingani kwa mapato na kusikilizwa Ulaya au Marekani. Ametoa onyo kwa wasanii wasiridhike na sifa za ndani pekee.



Kwenye chapisho jingine, Burna Boy alieleza tofauti kubwa ya mapato ya muziki nchini Nigeria na mataifa ya Magharibi. Alisema kusikilizwa mara milioni 1 nchini Nigeria huleta kati ya dola 300 hadi 400 pekee, ikilinganishwa na dola au paundi 3,000 hadi 4,000 kwa kiwango hicho hicho nchini Uingereza, Marekani au Ulaya.

Hali kama hii inaakisi pia Tanzania, ambapo wasanii wengi hutamba kwenye majukwaa ya ndani kama Boomplay na YouTube lakini hawapenyi kwenye chati za kimataifa kama Billboard, AppleMusic au SpotifyGlobal.

Tatizo ni kutegemea mashabiki wa ndani, ukosefu wa mitandao ya kimataifa, na uwekezaji mdogo kwenye ubora. Huu ni mwito kwa wasanii wa Afrika Mashariki kufikiria kimataifa kuwekeza kwenye ushirikiano wa nje, kujifunza masoko mapya, na kupambana kuwa sehemu ya jukwaa la dunia.

Share: