
Nyota wa mziki wa kizazi kipya kutoka mtwara ,ameonekana leo ndani ya baraza la sanaa la taifa
Ibraah ni msanii mwenye kesi ya madai ya shilingi Bilioni Moja anayo daiwa Hamonize ambae ni msanii mwenzake ,pia alikua boss wake katika kazi ya mziki yani ndio mwenye record lable ya KONDE Gang ambayo imemsajili na ilikuwa inasimamia kazi zake za mziki .
Leo tarehe 14 May 2025 ametua basata mapema tu ,licha ya mara ya kwanza msanii uyo kuonekana basata akiwa na wanasheria wake sakata lake lina husu kuvunja mkataba alio sajiliwa na konde gang ,sasa leo kaonekana kwa mara ya pili.Kama ilivyokuwa mara ya kwanza Ibraah ameonekana kuwa na tahadhari kubwa katika kuzungumzia yaliyojadiliwa ndani ya kikao hicho ambapo akiwa mbele ya Waandishi wa habari alizungumza kwa kifupi tu.
post ya msanii Ibraah kwenye mtandao wake wa kijamii
“Tumefanya mazungumzo lakini kikubwa naona tuwaachie Baraza la Sanaa mpaka watakapokuwa na uamuzi sahihi kuhusu hili na mimi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu tulipofikia ni pazuri zaidi.” — Ibraah
Asante sana kwa kuendelea kutembelea tovuti yetu kwa taarifa,matukio na mengine mengi utayapata hapa TOVUTI PENDWA
Kwa sasa bado haijafahamika rasmi ni lini uamuzi wa BASATA utatolewa lakini kinachoonekana ni kuwa pande zote zinaendelea kushirikiana kwa njia ya mazungumzo ili kufikia suluhu.