Zeco: zanzibar nzima inakosa umeme wakati huu kutokana na hitilafu iliyotokea tegeta, dar es salaam

limesema hitilafu imetokea katika mfumo wa gridi ya Taifa na hivyo kusababisha ukosefu wa huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo Tanzania Bara na Zanzibar

Shirika la Umeme Zanzibar ( ZECO) limesema Zanzibar nzima inakosa umeme wakati huu kutokana na hitilafu iliyotokea Tegeta, Dar es salaam katika mtambo wa kilovolti 132 wenye laini ya umeme kwenda Zanzibar kuanzia leo saa 7 mchana.

Taarifa ZECO imesema yafuatayo “Mpendwa Mteja kuna hitilafu ya umeme mkubwa mkondo wa kilovolt 132 kutokea Tegeta Tanzania Bara kuja Zanzibar kulikosababisha kuzimika umeme hafla maeneo yote ya Zanzibar, ZECO inaomba radhi kwa usumbufu unaoendelea kujitokeza, ahsanteni”

Nalo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema hitilafu imetokea katika mfumo wa gridi ya Taifa na hivyo kusababisha ukosefu wa huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo Tanzania Bara na Zanzibar na kwamba Wataalamu wanaendelea na jitihada za kuhakikisha huduma ya umeme inarejea katika hali yake ya kawaida “Shirika linawaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza”

Share: