Zao la bangi kuthibitishwa ohio marekani

Wakazi wa jiji la Ohio Marekani wamepiga kura kuidhinisha matumizi ya bangi kama kiburudisho 

Kulingana na NBC News, wapiga kura wa Ohio wamethibitisha Kwa kupiga kura nyingi kuhalalisha matumizi ya bangi Kwa burudani. Hii inaifanya Ohio kuwa jiji la 24 kuhalalisha matumizi ya bangi kutokana na hamasa ya kukua Kwa mazoea haya Kwa maeneo mengi ya ya nchi

Kura ya "ndio" inamaanisha watu walio na umri wa miaka 21 na zaidi katika jimbo hilo wataweza kutumia, kulima au kuuza bangi chini ya mpango wa udhibiti na kodi uliowekwa na serikali. Kipimo huanza kutumika ndani ya siku 30.

Share: