Zanzibar yaanza uchimbaji wa mafuta na gesi

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Shaaban Ali Othman leo ametangaza kukamilika kwa mchakato wa kuchakata data kutokea Tanzania Bara na sasa imeanza ugawaji rasmi wa maeneo (vitalu) kwa kazi ya uchimbaji wa mafuta na gesi Zanzibar kwenye maeneo yenye mafuta na gesi kwenye maeneo ya Bahari ya Zanzibar.

“Maandalizi yote husika yanayohitajika ili Zanzibar kuanza kutoa vitalu (maeneo) ya uwekezaji kwa ajili ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia yamekamilika, hii ina maana kwamba sasa Zanzibar iko tayari kwa duru ya kwanza ya utoaji vitalu na leseni katika maeneo ya baharini kwa Wawekezaji wa mafuta na gesi duniani kote.

Share: