Zanzibar: vat yaondolewa kwenye bidhaa ya sukari

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi ameondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye bidhaa ya sukari Zanzibar ili kuwasaidia Wananchi kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko kuu la Jumbi na Soko la samaki Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 26 Februari 2024 katika ziara yake maalumu alipotembelea masoko na kusikiliza changamoto zao.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewaomba Wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi kwa kupandisha mara mbili ya bei ili kuwasaidia Wananchi kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameisisitizia Taasisi ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi Zanzibar(ZEEA) kuwawezesha Wafanyabiashara wa soko la samaki Malindi kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza biashara zao.

Share: