Wb: bilioni 988.098 kutekeleza awamu ya 2 dmdp ii

Serikali ya Tanzania imetia saini Mkataba wa Tsh. Bilioni 988.098 kutoka Benki ya Dunia (WB), Fedha zitakazotumika kutekeleza Awamu ya 2 ya Mradi wa Miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP II)

Akizungumza mbele ya Mkurugenzi Mkazi wa WB, Nathan Belete, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ametaja maeneo yatakayofanyiwa Uboreshaji wa Miundombinu ni Ilala, Temeke na Kinondoni, Ubungo na Kigamboni. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Fedha, Awamu ya Kwanza ya DMDP iliyokamilika Mwaka 2203, Benki ya Dunia ilitoa Dola Milioni 300 (Tsh. Bilioni 760.5 zilizojenga Kilomita 207 za Barabara, Vituo 4 vya Mabasi, Kilomita 75 za Mfumo wa Maji na Mabwawa 3 ya kuzuia Mafuriko. 

Share: