Wajasiriamali wahimizwa kurasimisha biashara brela

MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Hashim Komba amewataka wajasiriamali wanaoshiriki katika maonesho ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, (BRELA) na wadau wake kutumia fursa hiyo kurasimisha biashara zao ili biashara zao ziweze kukua.

Mhe. Komba ametoa rai hiyo Oktoba 24, 2023 wakati akifungua Maonesho ya kwanza ya BRELA na wadau wake, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

“Wito wangu kwenu BRELA na wadau wengine wa maonesho haya ni kwamba tuhakikishe hawa wajasiriamali mbalimbali wanakua, hivyo wasaidiwe kwa kupatiwa elimu ili waweze kurasimisha biashara zao,” amesema Mhe. Komba.

Amesema ili kuboresha zaidi maonesho haya BRELA iendelee kuandaa maonesho kama haya katika maeneo mengine yatakayowezesha wadau wengi zaidi kufikiwa. Ameyataja maeneo ambayo yana idadi kubwa ya wajasiriamali katika Wilaya ya Ubungo kuwa ni Mbezi na Manzese, hivyo BRELA itoe kipaumbele kwa kuwapatia elimu kupitia maonesho kama haya.

Share: