Wafanyabiashara kisarawe walia na tra wasisitiza elimu ya mlipa kodi.

Ombi hilo lilitolewa na baadhi ya wafanyabishara wilayani humo, wakati wa mkutano wao na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabishara (JWT)

WAFANYABISHARA wilayani Kisarawe mkoani Pwani, wameiomba Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwapa elimu ya kutosha kuhusu ulipaji kodi wa hiari na matumizi ya mashine za EFD.

Ombi hilo lilitolewa na baadhi ya wafanyabishara wilayani humo, wakati wa mkutano wao na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabishara (JWT) wakiongozwa na Mwenyekiti wake Hamis Livembe, wakiwa kwenye ziara ya kikazi ya kusikiliza kero mkoani humo.

Mfanyabishara Christina Mulu, amesema TRA wanatakiwa kuwapa elimu ya kutosha kuhusu ulipaji kodi badala ya kukazania kukusanya bila kuwasikiliza wafanyabishara kwanza.

Mfanyabishara John Masine, amewataka TRA kuwasaidia wafanyabishara urahisi wa kupata kodi na kuwalinda kwa kuondoa wamachinga mbele ya fremu za biashara.

Share: