Mshauri mwelekezi kutoka Kampuni ya Quality Energy Development Consulting Limited (QED), Tony Deighton amesema mkataba huo umejikita katika pande mbili ambazo ni kifedha na sheria.
Wadau wa mafuta na gesi nchini wamekutana ili kujadili mkataba kifani wa mafuta na gesi, lengo likiwa ni kuwajengea uelewa na kutoa maoni kuhusu mkataba huo.
Semina hiyo imefanyika leo Novemba 30, 2023 Jijini Dodoma na kuwashirikisha Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya Msajili wa Hazina, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Mamlaka ya Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na Mamlaka ya Udhibiti, Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta Zanzibar (ZPRA).
Akizungumza wakati wa kuwasilisha mkataba huo, Mshauri mwelekezi kutoka Kampuni ya Quality Energy Development Consulting Limited (QED), Tony Deighton amesema mkataba huo umejikita katika pande mbili ambazo ni kifedha na sheria.
Amesema lengo la kuleta mkataba huo mbele ya wadau ni kutaka kupata maoni ya watu ili yaweza kutumika katika uboreshaji wa mkataba huo.
‘’Maoni haya yakishakusanywa kutoka kwa Wataalamu yataingizwa kwenye mkataba kifani wa mafuta na gesi kwa ajili ya kuvutia wawekezaji,“ amesema Deighton.