Uganda kuharibu chanjo za covid zenye thamani ya $7m

Zaidi ya dozi milioni 5.6 za chanjo za Covid-19 zilizonunuliwa kwa mkopo na serikali ya Uganda zimeisha muda wake, ripoti ya ukaguzi imesema.

Chanjo hizo zina thamani ya shilingi 28.1bn za Uganda ($7.3m; £5.8m) na zilinunuliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia.

Mamlaka inasema chanjo zilizokwisha muda wake zitaondolewa kwenye vituo vya afya na kuharibiwa. Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni Jumanne,

Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uganda John Muwanga pia alisema kuwa dawa nyingine zenye thamani ya $8.6m, nyingi zikiwa ni dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs), zimeisha muda wake baada ya kuondolewa na mabadiliko ya miongozo ya matibabu iliyopendekezwa na WHO.

Mamlaka yanatarajia hasara ya jumla kutoka kwa chanjo zilizoisha muda wake kuzidi $78m ifikapo mwisho wa mwaka huu.

"Mahitaji ya chanjo za Covid sasa ni sifuri. Hatupokei tena maagizo yoyote ya chanjo ya Covid.

Ikiwa hatuna watu wowote wanaohitaji au vituo vya afya vinavyohitaji chanjo hizi za Covid,

tunatarajia chanjo zaidi za covid itakwisha kwetu," mkuu wa wakala wa ununuzi wa dawa nchini Uganda Moses Kamabare aliambia shirika la utangazaji la umma la UBC.

Share: