Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa kazi ya uchorongaji wa visima vya Jotoardhi nchini Tanzania itaanza mwezi Aprili mwaka huu ili kuweza kuhakiki rasilimali ya Jotoardhi iliyopo kabla ya kuanza kwa shughuli za uzalishaji umeme kutokana na nishati hiyo.

Dkt. Biteko amesema hayo baada ya kutembelea vyanzo na mitambo ya kuzalisha umeme wa Jotoardhi katika Mji wa Naivasha, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya.

Amesema Tanzania kwa upande wake, tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya kuendeleza vyanzo vya Jotoardhi na kwamba kampuni ya KenGen mwezi Aprili mwaka huu itakuwa mkoani Mbeya kwa ajili ya kuanza uchorongaji vyanzo vya Jotoardhi katika eneo la Ngozi na Kiejo-Mbaka kwa kushirikiana na kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC).

Share: