Treni ya umeme (sgr) inatarajiwa kuanza safari kutoka jiji kuu la kibiashara dar es salaam kuelekea mkoa wa morogoro kwa muda wa saa 1

‘’Mafurushi makubwa hayataruhisiwa huku’’ - Msanja Kadogosa mkurugenzi mtendaji shirika la reli Tanzania TRC. 

Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania treni ya abiria ya umeme inatarajia kuanza safari zake rasmi kutoka jiji kuu la kibiashara Dar es salaam kuelekea mkoa wa Morogoro safari ambayo inatarajiwa kuwa ya saa moja na dakika arobaini na tisa badala ya saa tatu mpaka saa nne kwa gari.

Hii ni awamu ya kwanza ya safari hizo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR mpaka mji mkuu Dodoma. 

Share: