Trc: kutoka dar mpaka moro na treni ya sgr ni saa moja na nusu

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema hatua ya majaribio ya safari ya treni ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Morogoro leo ni muhimu kuelekea kuanza rasmi kwa safari za Dar - Dodoma July mwaka huu kama ilivyoagizwa na Rais Samia na kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwakuwa muda utakaotumika kusafiri Dar - Moro hautozidi dakika 90.

TRC, Mhandisi Machibya Shiwa amesema “Hatua ya leo kwetu ni muhimu kwamba tunafanya majaribio na inatuhakikishia kuanza safari mwaka huu na kama tulivyoelekezwa na Mh. Rais kwamba kufikia July safari ziwe zimeanza na naamini hadi July safari zitaanza Dar hadi Dodoma, hii ni hatua kubwa sana”

“Kwa namna ilivyosanifiwa itakapofika kiwango cha juu cha uendeshaji cha KM 160 kwa saa tutakuwa tunatumia chini ya dakika 90, haya ni majaribio na majaribio ni hatua lakini safari itachukua dakika 90”

Share: