Tfa yawahakikishia wakulima upatikaji wa pembejeo

Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA) kimesema kuwa kitahakikisha wakulima ambao ni wanachama wa chama hicho wanapata huduma bora za pembejeo za gharama nafuu za kilimo ikiwemo mbegu na mbolea kupitia maduka ya chama hicho yaliyopo katika mikoa mbali mbali ya Tanzania

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa TFA uliofanyika Jijini Arusha ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TFA Waziri Barnaba amesema kuwa chama hicho kitaendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wake ili waweze kufanya kilimo cha kisasa chenye tija na kukuza uchumi wao kupitia kilimo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TFA Jastin Shirima amesema kuwa chama hicho kitaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa wanachama wanafikiwa na mbolea za ruzuku kupitia matawi ya chama hicho yaliyotapaa kote nchini.

Share: