TBS imesema taratibu za uingizwaji wa chakula Nchini zilifuatwa ikiwemo ukaguzi na uchunguzi wa Kimaabara
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema Mchele, Mafuta ya kupikia ya Alizeti na Maharage ambavyo vimeongezwa Virutubisho vilivyotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani kwa ushirikiano na Taasisi ya Jumuiya za Kimataifa (Global Communities) kwa baadhi ya Shule za Dodoma, vyote ni salama kwa Walaji
TBS imesema taratibu za uingizwaji wa chakula Nchini zilifuatwa ikiwemo ukaguzi na uchunguzi wa Kimaabara
Meneja Uhusiano na Masoko wa TBS, Gladness Kaseka amesema "Utaratibu wa kuongeza virutubisho kwenye chakula (Food Fortification) unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji."
Siku chache zilizopita Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema Taasisi hiyo ya Marekani inunue vyakula kutoka kwa Wakulima wa Tanzania na Virutubisho viwekwe huku Watanzania wakishuhudia