Tanzania yapokea tsh. bilioni 750.7 kwaajili ya huduma za maji vijijini

Benki ya Dunia imeipa Tanzania Dola Milioni 300 (Tsh. Bilioni 750.7) ili kupanua wigo wa utekelezaji kufikia Mikoa 25, ambapo kwa sasa Tsh. Milioni 970 zimepelekwa katika Halmashauri zote kwa ajili ya kuanza utekelezaji

Awali Tanzania ilipata Dola Milioni 350 (Tsh. Bilioni 875. katika miaka mitano kutekeleza Programu ya Uendelevu wa Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini kutoka Benki ya Dunia na kuelezwa ndani ya Miaka mitatu ya kwanza ilifanikisha kufikisha maji kwa zaidi ya watu wapya Milioni 4.7 Vijijini katika Mikoa 17.

Share: