Tanzania na Rwanda zimekubaliana kwa pamoja kuweka mazingira bora ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya Bandari ya Dar es salaam ikiwa ni miongoni mwa njia za kukuza uchumi wa Nchi hizi mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba ameyasema haya leo kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari Kigali Rwanda akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Rwanda Vicent Biruta ambapo hatua hii imekuja baada ya Rwanda kuongeza wigo wa matumizi ya Bandari ya Dar es salaam kwa zaidi ya 80% kwa usafirishaji wa mizigo yake.
Waziri Makamba ambaye yupo Rwanda kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, pia amejadiliana na Waziri Biruta masuala mengine yanayozihusu Nchi hizi mbili ikiwemo mradi wa umeme wa Maporomoko ya Mto Rusumo, Kilimo na Teknolojia.