Takukuru: serikali yataifisha mali zenye thamani ya tsh. bilioni 2.14

Mali zenye thamani ya Tsh. Bilioni 2.14 zikijumuisha Nyumba, Viwanja na magari ambazo zilizohusishwa na tuhuma za Rushwa zilitaifishwa na Serikali kati ya Machi 19, 2021 hadi Machi 18, 2024. 

Ripoti ya TAKUKURU imeeleza Miradi ya Maendeleo 3,576 yenye thamani ya Tsh. Trilioni 16.76 ilifuatiliwa na ushahidi ulipopatikana kwa kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kesi zilifunguliwa na kupelekwa Mahakamani. 

Kesi 1,922 za Rushwa ziliendeshwa na Mahakama ilitoa maamuzi katika kesi 1,303 huku Jamhuri ikishinda kesi 801 sawa na 61%, baada ya washtakiwa kupatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo jela au kulipa faini. 

Share: