Inadhaniwa kuwa unywaji wake uliongezeka wakati wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya, na kusababisha vifo vya idadi isiyojulikana ya watu.
Mamlaka katika jimbo la Ikweta ya Kati nchini Sudan Kusini imepiga marufuku uuzaji wa bia maarufu baada ya watu kadhaa kufariki baada ya kunywa pombe hiyo ya kienyeji.
Royal Gin, maarufu kama "Makuei Gin" inasemekana kuwa na uraibu, haswa kwa vijana.
Inadhaniwa kuwa unywaji wake uliongezeka wakati wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya, na kusababisha vifo vya idadi isiyojulikana ya watu.
"Nimepiga marufuku bia hii nyekundu, Royal Gin inayoitwa 'Makuei'. Hakuna mtu anayepaswa kuiuza wala kuinywa kwa sababu inaua vijana wengi," Gavana wa jimbo la Central Equatoria Emmanuel Adil Anthony alisema Jumapili.
“Vijana wengi wanapolewa huwapiga mama zao kwa mapanga,” aliongeza.
Kanisa la Kianglikana katika mji mkuu, Juba, limemtaka gavana huyo kuhakikisha marufuku hiyo inatekelezwa.
Bia hiyo ilipewa jina la utani la Waziri wa Habari Michael Makuei mnamo 2019, ambaye anasemekana kuwa waziri mzungumzaji zaidi nchini Sudan Kusini.
Mwaka jana, waziri alitoa wito wa kupigwa marufuku kwa bia hiyo na kutaka kiwanda kinachoizalisha kifungwe.