
Tunafuraha kubwa kukufikishia taarifa , hii ni kwa wafanya biashara wote wa ndani na njee ya nchi.
East Africa community and logistics ni Kituo cha kisasa cha Biashara na usafirishaji cha EACLC kilichojengwa Ubungo Jijini Dar es salaam sasa ujenzi umekamilika na sasa Wafanyabiashara wa Tanzania ambao walishalipia kodi ya pango kwa ajili ya kumiliki Maduka “fremu” ndani ya Kituo hicho wameanza rasmi kukabidhiwa funguo za Maduka yao.
Akizungumza na Waandishi wakati wa makabidhiano hayo Afisa masoko wa @eaclc_official Linda Mtui amesema Uongozi wa Kituo hicho umefurahishwa na muitikio mkubwa wa Wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza kukodi fremu hizo na kusisitiza kuwa bado zimebaki chache hivyo Wafanyabiashara wachangamkie.
- Kituo hiki ambacho kina Maduka yasiyopungua elfu mbili ( 2000), eneo maalum la Mabenki zaidi ya 10, migahawa ya kisasa na maegesho ya magari yanayoweza kupokea magari zaidi ya elfu moja kwa wakati mmoja, kinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni ambapo kodi ya fremu moja kwa mwezi inaanzisha shilingi milioni moja ( 1,000,000 ).
“Tunayofuraha pia kuwaeleza Watanzania kuwa Mabasi ya Mwendokasi yataanza kufanya safari kutoka Gerezani Kariakoo hadi hapa EACLC moja kwa moja kila siku, tunawakaribisha pia Wafanyabiashara kuja kutembea na kujionea fremu hizi na muundo huu wa kisasa kabisa kwa Kituo cha Biashara, watupigie kwenye 0753-669-724” ——— Linda Mtui, Afisa Masoko