Soko la uhakika zao la mwani zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amemhakikishia Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar na ujumbe wake kuwa Serikali ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Nutri-Sun Limited kutoka Uingereza katika kukamilisha mradi wa kiwanda cha kuchakata mwani kilichopo Chamanangwe, Pemba ambacho kukamilika kwake kutawanufaisha kwa kurahisisha kupata soko la uhakika.

Katika salamu zake naye Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar amemweleza Rais Dk. Mwinyi kwamba mipango ya kupata mashine na teknolojia ya kuchakata mwani imekamilika hivyo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024 kiwanda hicho kitaanza kuzalisha “Carrageenan” ambayo itatatumika kwa matumizi ya viwanda vya chakula na matibabu.

Aidha, Bi. Marisa Drew kutoka benki ya Standard Chartered alimhakikishia Rais Dk. Mwinyi upatikanaji endelevu wa fedha ambazo zitatumika kununulia mashine na zao la mwani, kiwanda hicho kitawawezesha wakulima wa mwani hasa wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi.

Rais Dk.Mwinyi amekutana na ujumbe huo tarehe: 19 Februari 2024 Ikulu Zanzibar.

Share: