Sgr: serikali haidaiwi na mkandarasi yeyote kwenye kazi zilizofanyika

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa akizungumzia gharama zilizotumika kwenye ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) amesisitiza Serikali haidaiwi na Mkandarasi yeyote kwenye kazi zilizofanyika.

Kuhusu migomo ya mara kwa mara ya Wafanyakazi wa Mradi, amesema "Hivyo ni vitu vya kawaida ambavyo tunakumbana navyo kwenye Mradi na kimsimgi tunavimaliza. Pia, maeneo ambayo Wafanyakazi wengi wanapunguzwa sababu ni mradi kukamilika kwa asilimia kubwa sehemu husika.”

Share: