Serikali yajivunia mfumo wa kidijitari wa manunuzi ya umma ( nest) yaziba mianya ya rushwa

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete anesema eneo la ununuzi wa umma limekuwa likiripotiwa kugubikwa na vitendo vya rushwa na ubadhirifu ambapo zaidi ya asilimia 72 ya bajeti ya Serikali imekuwa ikitumika kwenye manunuzi hayo ya umma 

Amesema kutokana na uzito huo Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao imeamua kusanifu, kujenga na kusanikisha Mfumo wa Kitaifa wa Kielektroniki wa Ununuzi Tanzania {National e-Procurement System of Tanzania (NeST)} ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo. 

Mhe.Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha wakati akifunga kongamano la 14 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi zaidi ya 900 lenye kauli mbiu "Mabadiliko ya kidijitali kwa ajili ya kuboresha usimamizi na ugavi kelekea maendeleo endelevu"

Amesema mfumo huo utasaidia kuondoa mianya ya rushwa na upendeleo na hivyo thamani ya pesa za Serikali katika bidhaa na huduma italindwa kwani kutakuwa hakuna ulazima wa watu kukutana ana kwa ana

Mhe.Kikwete amesema u mfumo huo utaongeza ufanisi, uwazi na ushindani katika ununuzi wa umma. 

Katika hatua nyingine, Mhe.Kikwete amesema serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayesababisha upotevu wa rasilimali za nchi huku akiwataka wasithubutu kucheza na mfumo huo mpya wa manunuzi kwa umma.

Aidha, ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wataalam wenu wamesajiliwa na wanazo sifa za kufanya kazi za ununuzi na ugavi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kupitia mfumo.

Share: