Serikali ya kenya imeanza rasmi azma ya kuongeza tozo ya barabarani hatua ambayo inatarajiwa kupandisha bei ya petroli na dizeli

Upinzani umepinga pendekezo hilo ukitaka litupiliwe mbali endapo litawasilishwa kwa namna yoyote

Kulingana na Gazeti la The Star, Wizara ya Barabara na Uchukuzi imetoa wito kwa umma kutoa maoni kuhusu azma yake ya kubadilisha sheria iliyoweka tozo hiyo kuwa Shilingi 18 kwa lita ya petroli na dizeli mwaka wa 2016, na kupendekeza tozo ya juu zaidi.

"Wizara ya Barabara na Uchukuzi inapendekeza marekebisho ya [agizo] kwa kuongeza tozo ya matengenezo ya barabara kwenye petroli na dizeli," ilani hiyo imeangaziwa katika magazeti inasema.

Wizara hiyo imeandaa kongamano mbalimbali za ushiriki wa umma katika miji ya Nairobi, Nyeri, Eldoret, Nakuru, Isiolo, Machakos, Kisumu, Garissa na Mombasa kuanzia tarehe 8, Julai.

Hivi majuzi, Waziri Kipchumba Murkomen aliwasihi wabunge kuzingatia kuidhinisha nyongeza ya Sh7 kwa lita, na hivyo kupandisha kiwango kipya hadi Sh25 kwa lita.

Alisema lengo ni kuziba pengo la fedha za kutengeneza barabara, akisema makusanyo ya sasa ambayo wastani wa shilingi bilioni 80 za Kenya kwa mwaka hayatoshi.

Upinzani umepinga pendekezo hilo ukitaka litupiliwe mbali endapo litawasilishwa kwa namna yoyote (katika Muswada wa Sheria ya Fedha au kama agizo la ushuru).

Share: