Serikali kulipa zaidi ya tsh. bilioni 144 kuwafidia wakazi waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa julius nyerere

Serikali imesema inatafuta Fedha zitakazotumika kuwafidia Wakazi waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere katika eneo la Kipunguni Jijini Dar es Salaam, ambao madai yao yamehakikiwa

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema “Sasa, tunaendelea kutafuta fedha, ndani ya mwaka huu wa fedha unaoendelea ili kuweza kuanza kufanya malipo hayo.”

Aidha, ameongeza kuwa tathmini mpya ya ardhi na mali iliyofanyika kwa Wakazi 1,184 inaonesha Serikali italipa zaidi ya Tsh. Bilioni 144, ikiwa ni tofauti na tathmini ya Mwaka 2009 iliyoonesha malipo yalipaswa kuwa Tsh. Bilioni 15.5. 

Share: