Serikali kujenga kampasi 14 mikoa ya pembezoni

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali iko kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa kampasi 14 mpya za vyuo vikuu kwenye mikoa ya pembezoni isiyokuwa na vyuo vikuu. 

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Kigoma, Ruvuma, Singida, Mwanza, Kagera, Tanga, Njombe, Tabora, Manyara, Simiyu, Shinyanga, Lindi, Rukwa, na Katavi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 30, 2023) wakati akizungumza na wahadhiri na wahitimu kwenye mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu cha Iringa yaliyofanyika chuoni hapo amako pia alimwakilisha Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan.

“Hatua hiyo ni moja ya jitihada za makusudi za Serikali za kuharakisha ukuaji wa uchumi kwenye maeneo ya pembezoni, kuongeza nafasi za elimu ya ufundi, ujuzi na stadi za maisha katika maeneo hayo ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa fursa za elimu na ajira.”

Akielezea uboreshaji wa miundombinu ya vyuo vikuu, Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inaendelea na ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo ni vyumba vya mihadhara, maabara, nyumba za walimu na maktaba.

Share: