Serikali imetumia tsh. trilioni 10.69 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa (sgr)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia Tsh. trilioni 10.69 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa yenye urefu wa kilometa 1,219 kuanzia Dar es Saalam hadi Mwanza.

Akielezea utekelezaji wa miradi nane ya kielelezo kwa mwaka 2023/2024 Bungeni leo Jumatano, Aprili 3, 2024, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Februari 2024, ujenzi wa reli hiyo umefikia viwango vya kati ya asilimia 5.38 na asilimia 98.84, tayari reli hiyo imeshaanza kufanyiwa majaribio kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Kama nyote mlivyoshuhudia, majaribio ya treni hiyo ya mwendo kasi yalifanyika kwa mafanikio makubwa mwezi Februari, 2024. Ni matarajio yetu kuwa huduma ya usafiri na usafirishaji itaanza ifikapo Julai, 2024 kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Dodoma,” amesema Waziri Mkuu wakati akiwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2023/2024 na Mwelekeo wa Kazi zake kwa mwaka 2024/2025.

“Ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (52.69, Makutupora - Tabora (Kilomita 371) umefikia asilimia 13.86, Tabora - Isaka (Kilomita 165) umefikia asilimia 5.38 na Tabora – Kigoma (Kilomita 506) umefikia asilimia 1.81 Kilomita 300) umefikia asilimia 98.84, Morogoro – Makutupora (Kilomita 422) umefikia asilimia 96.35”




Share: