Serikali imekamilisha malipo ya shilingi bilioni 753 ya ndege tatu aina ya boeing 737-9 max zitakazowasili aprili, 2024

“Serikali imekamilisha malipo ya shilingi Bilioni 753 kwa ajili ya ndege tatu aina ya Boeing 737-9 Max (ndege mbili) na Boeing 787-8 (ndege moja). Ndege mbili aina ya Boeing 737-9 Max zimewasili nchini Oktoba, 2023 na Machi, 2024 na nyingine moja inategemewa kuwasili Aprili, 2024 na hivyo kulifanya Shirika hilo kuwa na jumla ya ndege 16. Ndege hizo zitawezesha kuongeza safari za ndani na nje ya nchi na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi kama vile utalii, biashara, kilimo, mifugo na uvuvi.”  

Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akisoma hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha wa 2024/2025 Bungeni jijini Dodoma.

Share: