kama Wawekezaji wana changamoto yupo tayari kujadiliana nao ili kuzitatua huku viwanda vikiwa vinaendelea na uzalishaji.
Serikali imegoma kuridhia ombi la kufungwa kwa Kiwanda cha chai cha Mo Enterprises na Viwanda vingine kadhaa Nchini ili kuepusha athari ikiwemo Watu kupoteza ajira.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiwa Dodoma leo, amesema kama Wawekezaji wana changamoto yupo tayari kujadiliana nao ili kuzitatua huku viwanda vikiwa vinaendelea na uzalishaji.
“Nimepokea barua ya kampuni ya Mohamed Enterprise kutaka kufunga Viwanda nimewaambia hawawezi kufunga viwanda, tujadiliane njia nyingine lakini sio kufunga kwasababu kwetu bado sekta ya chai bado ni muhimu kwa ajira za Watu, binafsi naamini nikienda Rungwe kama Wakulima wangekuwa hawana mazao mengine umasikini ungekuwa mkubwa mno kwa hali ya chai ilivyo, Lupembe, Mafinga, Mufindi kote hali ingekuwa mbaya”
“Nimepokea maombi ya MO kuja kwetu Serikali kwamba Serikali tuyachukue mashamba (ili kuyaendeleza) tutaunda Timu itaenda kuyakagua tutaangalia thamani halisi ya wakati huu kwasababu hayakutunzwa vizuri mashamba wala vile Viwanda kwa muda mrefu sana kwahiyo tutaangalia njia zote lakini sekta ya chai itaendelea kuwa hai, nimeagiza hakuna kufunga kiwanda lazima waendeele na uzalishaji hilo ni la lazima kisha tutakaa chini kujadiliana mambo mengine”
“Nawahakikishia ninaendelea na majidiliano na Wizara ya Fedha ili tuwe na njia bora kupima viwango vya tozo, nimeongea na Waziri wa Uwekezaji ili hivi viwanda vipate nafuu ya kodi ya kuagiza nje kwasababu kama tunampa Mtu wa Export sehemu nafuu ya kodi, ukitazama sekta ya chai kwa ujumla bidhaa zake zinahusisha kusafirisha nje”
“Nimekaa na Timu ya Wataalamu imenifanyia uchambuzi wa bei ya majani mabichi ya chai, kwa namba inatakiwa bei ishuke lakini nimewaambia bei ya Mkulima haitoshuka tuta-mantain bei ya mwaka jana” —— amesema Waziri wa Kilimo