Mwaka 2022 madini yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 3,395.3 yaliuzwa nje ya nchi sawa na asilimia 56 ya mauzo yote
Ukuaji wa sekta ya madini na mchango wake kwenye pato la Taifa umeendelea kuimarika na hivyo kuongezeka kutoka asilimia 4.4 mwaka 2017 hadi asilimia 7.2 mwaka 2021.
Kulingana na serikali ya Tanzania mwenendo huu unatoa tumaini kuwa sekta ya madini itaweza kuchangia hadi asilimia kumi kwenye pato la Taifa kufikia mwaka 2025 kama lilivyo kusufi la Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025.
Mwaka 2022 madini yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 3,395.3 yaliuzwa nje ya nchi sawa na asilimia 56 ya mauzo yote ya bidhaa zilizouzwa nje ya nchi.
Wakati hayo yanafanyika wafanyabiashara ya madini kwenye soko la madini mkoani Arusha wamemuambia Mkuu wa mkoa Mh. Paul Christian Makonda kwamba endapo baadhi ya mambo yatafanyika sekta hiyo ya Madini inaweza pia kukuza uchumi wa Arusha kwa asilimia kubwa zaidi na hivyo kuweka msawazo na mzunguko mkubwa wa fedha.