Ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali imebaini matukio yasiyofaa ya mifumo ya fedha katika mashirika yote ya serikali

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Mifumo ya TEHAMA kwa Mwaka wa Fedha 2022/23, imeonesha Wizara ya Fedha ilibainika kuwa na Malipo yaliyoingizwa kwenye leja ya jumla bila Mikataba ya manunuzi.

Pia, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilizalisha bili za Kiotomatiki zinazozidi Tsh. Bilioni 1.4 kupitia moduli ya "bili nyinginezo" yenye uangalizi mdogo, na ukosefu wa ufuatiliaji sahihi wa vibali vilivyolipwa kupitia moduli hiyohiyo.

Katika hali kama hiyo, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) pia ilitengeneza bili kwa njia ya kawaida ambazo zilipaswa kuwa za kiotomatiki, na hivyo kusababisha upotevu wa mapato.

Share: