Ripoti ya (cag) imeeleza kuwa mwaka wa fedha wa 2022/23 chama cha wananchi (cuf) kilipata hati yenye shaka

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/23 inaeleza Chama cha Wananchi (CUF) kilipata hati yenye shaka huku Chama cha National Reconstruction Alliance kikipata hati mbaya

Pia, CAG alishindwa kutoa maoni kwa Chama cha Alliance for African Farmers na Chombo cha Watoa Huduma ya Maji - Utegi kutokana na kutojumuishwa kwa taarifa linganifu na kutojitosheleza kwa nyaraka kuthibitisha usahihi wa matumizi yaliyofanyika

CAG ameeleza jambo hilo ni kinyume na matakwa ya Aya ya 26 na 27 ya IPSAS 17 (Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu katika Taasisi za Umma) na Kanuni ya 22(1) ya Kanuni za Uandaaji wa Taarifa za Fedha za Vyama vya Siasa za Mwaka 2019

Share: