Rc chalamila apokea wageni kutoka finland na un-women

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amepokea wageni maalum kutoka Finland na UN-WOMEN Ofisini kwake Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.

Akipokea wageni hao RC Chalamila ameishukuru Serikali ya Finland kwa mashirikiano katika nyanja mbalimbali na Tanzania hususani Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema Mkoa huo una fursa nyingi za uwekezaji na vivutio mbalimbali pia idadi ya watu ni kubwa, ulinzi na usalama madhubuti vilevile wakazi wake ni wakarimu sana.

Aidha Mhe Chalamila amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua nchi na Kuimarisha Diplomasia na mataifa mbalimbali Duniani hivyo ujio wao unadhihirisha pasina shaka umahiri wa Dkt Samia katika Kuimarisha Demokrasia Duniani.

Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Rehema Madenge amesema Jiji hilo ni la kibiashara katika Tanzania ni moja kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara hivyo anawakaribisha sana katika mashirikiano ya kiuongozi, na hata kiuchumi kwa masilahi mapana ya watu wote kutoka mataifa hayo mawili.

Share: