Rais wa romania atawasili nchini kwa ziara ya kibiashara

Rais wa Romania, Klaus Iohannis, anatarajia kufanya nchini kuanzia kesho November 16 hadi 19, 2023 kwa mwaliko wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Romania.

Kupitia ziara hii Tanzania na Romania zimedhamiria kuinua na kuimarisha kiwango cha biashara kati ya Nchi hizi mbili licha ya Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake nchini Romania, kiwango cha biashara kati ya mataifa haya mawili bado ni kidogo na kimeshuka katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na fursa za kibiashara zilizopo.

Mathalani mwaka 2021 Tanzania iliuza Romania bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 7.9 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo iliuza bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 4.06, pia Romania ilinunua bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 11.6 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo ilinunua bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 2.4

Share: