Rais samia suluhu ametoa msamaha kwa wateja wa mamlaka za maji kuondoa faini ili waanze kulipia kidogokidogo

Rais Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara ya Maji kupitia Mamlaka za Maji kuondoa faini kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa Wateja wake ili waanze kulipia kidogokidogo sehemu ya madeni yao halisi na kuagiza pia warejeshewe huduma ya maji wakati wakiendelea kupunguza madeni.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameyasema haya March 26,2024 Dodoma kwenye kikao kazi na Viongozi wa Watendaji wa Sekta ya Maji ikiwa ni pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Maji, Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka zote za maji pamoja na Mameneja wa RUWASA kwa lengo la kuendelea kukumbushana na kuelezana kwa msisitizo wajibu wa Sekta katika kufanikisha utendaji kazi, utoaji huduma na utekelezaji wa miradi ya maji inayoendelea hapa Nchini.

“Tunatoa mwezi mmoja Mwananchi ambaye umekatiwa maji kwasababu ya faini umechelewa kulipa na umekatiwa maji, faini tunasamehe kwa mwezi mmoja kupitia maelekezo ya Mh. Rais, sasa chelewachelewa utamkuta Mwana sio wako, hata kama una kideni kikubwa niwaombe Watendaji wekeni utaratibu ili Mtu awe anapunguza kidogokidogo huku anapata huduma”

Aweso amewataka pia Watendaji wote wa Mamlaka za Maji na Bodi zake kuwa kipimo cha ufanisi katika kazi kitakua katika maeneo ya kudhibiti upotevu wa maji pamoja na kutochelewesha maunganisho mapya kwa Mteja mwenye kutaka huduma ya Maji.

Share: