Rais mwinyi na rc makonda kwenye semina ya wanahisa wa crdb

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Nsekela wamewasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa Mjini Arusha AICC kuhudhuria semina ya wanahisa wa Benki ya CRDB.



Semina hii ni utangulizi wa Mkutano mkuu wa 29 wa wanahisa wa Benki hiyo ikiwa ni utamaduni wa Benki hiyo kila Mwaka ili kujadili masuala mbalimbali ya Benki hiyo, Mkutano unaotarajiwa kufanyika mjini Arusha Jumamosi ya Mei 18, 2024.

Kufanyika kwa semina na Mikutano hii inatarajiwa kuhudhuriwa na Wanachama wa Benki hiyo na Maafisa mbalimbali wa CRDB wanaokadiriwa kufikia zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, suala ambalo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda anaamini kuwa Mikutano hii ni fursa ya Wana Arusha na wafanyabiashara mbalimbali kunufaika na ujio wa ugeni huo.


Kaulimbiu ya Semina ya Wanahisa inasema "Ustawi pamoja"

Share: