Prof. sospeter mwijarubi muhongo ametaja vyanzo vipya vinavyoweza kuondoa tatizo la upungufu wa umeme nchini

Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye kwasasa ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijni Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo ametaja vyanzo vipya vya uhakika vinavyoweza kuondoa tatizo la upungufu wa umeme Nchini.

Prof. Muhongo amesema hayo wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni umeme wa jua, umeme wa upepo na umeme unaotokana na joto ardhi ambao Nchi Jirani ya Kenya imefanikiwa kuzalisha umeme huo kwa kiwango kikubwa.

“Nawathibitishia vyanzo vya uhakika kuwa jua linavyopiga ardhini square meter moja unapata bulb tatu au nne za umeme yaani ni waltz 342 nataka kuwaonesha kwanini Tanzania tunatakiwa kwenda huko sasa hivi na hii sisemi msiache mengine nachukulia mfano wa India na China, aina ya pili ni upepo na upepo ambao unaweza kuzalisha umeme lazima speed yake iwe mita nne kwa sekunde ikiwa 50 au 60 kama speed ya gari uzalishaji unakuwa ni mkubwa sana kwa Afrika tujifunze kwa wenzetu Wakenya wao wana umeme mwingi zaidi wanaongoza kwa Afrika wana MW 440”

Share: